First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى
النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ
Swahili
Alif Lam Ra. (A.L.R.) Hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu
kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe
kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa,
|
Ayah 14:2 الأية
اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ
لِّلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ
Swahili
Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na
ardhi. Na ole wao makafiri kwa adhabu kali!
|
Ayah 14:3 الأية
الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن
سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُولَٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ
Swahili
Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu
wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali.
|
Ayah 14:4 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ
فَيُضِلُّ اللَّهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ
الْحَكِيمُ
Swahili
Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi
Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni
Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
|
Ayah 14:5 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ
الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَذَكِّرْهُم بِأَيَّامِ اللَّهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ
لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ
Swahili
Na tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe watu wako kwenye
giza uwapeleke kwenye mwangaza. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika
katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.
|
Ayah 14:6 الأية
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ
أَنجَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ
أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن
رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ
Swahili
Na Musa alipo waambia watu wake: Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu aliyo
kujaalieni, pale alipo kuokoeni kutokana na watu wa Firauni walio kupeni adhabu
mbaya kabisa, wakiwachinja wenenu wanaume, na wakiwawacha hai wanawake. Na
katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unao toka kwa Mola wenu Mlezi.
|
Ayah 14:7 الأية
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن
كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ
Swahili
Na alipo tangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni; na mkikufuru,
basi adhabu yangu ni kali.
|
Ayah 14:8 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ إِن تَكْفُرُوا أَنتُمْ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا فَإِنَّ
اللَّهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ
Swahili
Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote waliomo duniani, hakika Mwenyezi Mungu
ni Mkwasi, Anajitosha, Msifiwa.
|
Ayah 14:9 الأية
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ
ۛ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّهُ ۚ جَاءَتْهُمْ
رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا
إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا
تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ
Swahili
Je! Hazikukufikieni khabari za walio kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na A'adi, na
Thamud, na walio baada yao, ambao hapana awajuaye ila Mwenyezi Mungu? Mitume wao
waliwajia kwa hoja zilizo wazi, na wao wakarudisha mikono yao kwenye vinywa
vyao, wakasema: Hakika sisi tumeyakataa hayo mliyo tumwa, na hakika sisi tuna
shaka kubwa na mnayo tuitia.
|
Ayah 14:10 الأية
قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ
يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ
مُّسَمًّى ۚ قَالُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن
تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Swahili
Mitume wao wakasema: Ati pana shaka na Mwenyezi Mungu, Muumba mbingu na ardhi?
Yeye anakuiteni apate kukufutieni madhambi yenu, na akupeni muhula mpaka muda
ulio wekwa. Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni wanaadamu kama sisi. Mnataka
kutuzuilia na waliyo kuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja ilio wazi.
|
Ayah 14:11 الأية
قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَٰكِنَّ
اللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن
نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ وَعَلَى اللَّهِ
فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ
Swahili
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote ila ni wanaadamu kama nyinyi.
Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake. Wala sisi
hatuwezi kuleta uthibitisho ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi
Mungu ndio wategemee Waumini.
|
Ayah 14:12 الأية
وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا ۚ
وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَا آذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ
الْمُتَوَكِّلُونَ
Swahili
Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye
Njia zetu. Na hapana shaka sisi tutayavumilia hayo maudhi mnayo tuudhi. Na juu
ya Mwenyezi Mungu wategemee wanao tegemea.
|
Ayah 14:13 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَا أَوْ
لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۖ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ
الظَّالِمِينَ
Swahili
Na walio kufuru wakawaambia Mitume wao: Tutakutoeni katika nchi yetu, au mrudi
katika mila yetu. Basi Mola wao Mlezi aliwaletea wahyi: Hakika tutawaangamiza
walio dhulumu!
|
Ayah 14:14 الأية
وَلَنُسْكِنَنَّكُمُ الْأَرْضَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَافَ مَقَامِي
وَخَافَ وَعِيدِ
Swahili
Na tutakuwekeni katika ardhi baada yao. Haya ni kwa anaye ogopa kusimamishwa
mbele yangu, na akaogopa maonyo yangu.
|
Ayah 14:15 الأية
وَاسْتَفْتَحُوا وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ
Swahili
Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi,
|
Ayah 14:16 الأية
مِّن وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيُسْقَىٰ مِن مَّاءٍ صَدِيدٍ
Swahili
Ambaye nyuma yake ipo Jahannamu, na atanywishwa maji ya usaha.
|
Ayah 14:17 الأية
يَتَجَرَّعُهُ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُ وَيَأْتِيهِ الْمَوْتُ مِن كُلِّ مَكَانٍ
وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ ۖ وَمِن وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ
Swahili
Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila
upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vile vile.
|
Ayah 14:18 الأية
مَّثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ
الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ ۖ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ
ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ
Swahili
Mfano wa walio mkufuru Mola wao Mlezi - vitendo vyao ni kama jivu linalo
peperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya mdharba. Hawawezi kupata chochote
katika waliyo yafanya. Huko ndiko kupotelea mbali!
|
Ayah 14:19 الأية
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِن
يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ
Swahili
Huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka
atakuondoeni na alete viumbe wapya!
|
Ayah 14:20 الأية
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ بِعَزِيزٍ
Swahili
Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu.
|
Ayah 14:21 الأية
وَبَرَزُوا لِلَّهِ جَمِيعًا فَقَالَ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا
كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ اللَّهِ مِن
شَيْءٍ ۚ قَالُوا لَوْ هَدَانَا اللَّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ۖ سَوَاءٌ عَلَيْنَا
أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ
Swahili
Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia walio
takabari: Sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika
adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli tuongoa basi
hapana shaka nasi tungeli kuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri;
hatuna pa kukimbilia.
|
Ayah 14:22 الأية
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ
الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن
سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي
وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ
إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ
عَذَابٌ أَلِيمٌ
Swahili
Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi
ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu
yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali
jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa
watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi
Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu.
|
Ayah 14:23 الأية
وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن
تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ
فِيهَا سَلَامٌ
Swahili
Na walio amini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kati
yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkio yao humo yatakuwa:
Salaam!
|
Ayah 14:24 الأية
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ
طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ
Swahili
Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti
mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni.
|
Ayah 14:25 الأية
تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّهُ
الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Swahili
Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu
huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka.
|
Ayah 14:26 الأية
وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ
مَا لَهَا مِن قَرَارٍ
Swahili
Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng'olewa juu ya ardhi. Hauna imara.
|
Ayah 14:27 الأية
يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ
الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ
اللَّهُ مَا يَشَاءُ
Swahili
Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya
dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu.
Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
|
Ayah 14:28 الأية
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا
قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ
Swahili
Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na
wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo?
|
Ayah 14:29 الأية
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا ۖ وَبِئْسَ الْقَرَارُ
Swahili
Nayo ni Jahannamu! Maovu yaliyoje makaazi hayo!
|
Ayah 14:30 الأية
وَجَعَلُوا لِلَّهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ ۗ قُلْ تَمَتَّعُوا
فَإِنَّ مَصِيرَكُمْ إِلَى النَّارِ
Swahili
Na walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili wapoteze watu kwenye Njia yake.
Sema: Stareheni! Kwani marejeo yenu ni Motoni!
|
Ayah 14:31 الأية
قُل لِّعِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا يُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُنفِقُوا مِمَّا
رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ
فِيهِ وَلَا خِلَالٌ
Swahili
Waambie waja wangu walio amini, washike Sala, na watoe katika tulivyo waruzuku,
kwa siri na dhaahiri, kabla haijafika Siku isiyo kuwa na biashara wala urafiki.
|
Ayah 14:32 الأية
اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً
فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ
لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka
mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya
yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito
ikutumikieni.
|
Ayah 14:33 الأية
وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ دَائِبَيْنِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ
وَالنَّهَارَ
Swahili
Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na
mchana kwa manufaa yenu.
|
Ayah 14:34 الأية
وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّهِ لَا
تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ
Swahili
Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi
kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.
|
Ayah 14:35 الأية
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي
وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ
Swahili
Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na
uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.
|
Ayah 14:36 الأية
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ
مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza watu wengi. Basi aliye nifuata
mimi huyo ni wangu, na aliye niasi, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
|
Ayah 14:37 الأية
رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ
بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ
النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ
يَشْكُرُونَ
Swahili
Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde
lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili
washike Sala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda,
ili wapata kushukuru.
|
Ayah 14:38 الأية
رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ ۗ وَمَا يَخْفَىٰ عَلَى
اللَّهِ مِن شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ
Swahili
Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayo yaficha na tunayo yatangaza. Na
hapana kitu kinacho fichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika
mbingu.
|
Ayah 14:39 الأية
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ
إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ
Swahili
Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu
Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi.
|
Ayah 14:40 الأية
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ
دُعَاءِ
Swahili
Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu
pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu.
|
Ayah 14:41 الأية
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ
Swahili
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya
kusimama hisabu.
|
Ayah 14:42 الأية
وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ ۚ إِنَّمَا
يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ
Swahili
Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika
Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.
|
Ayah 14:43 الأية
مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ ۖ
وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ
Swahili
Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu.
|
Ayah 14:44 الأية
وَأَنذِرِ النَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ الْعَذَابُ فَيَقُولُ الَّذِينَ ظَلَمُوا
رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ
الرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوا أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ
Swahili
Na waonye watu siku itapo wajia adhabu, na walio dhulumu waseme: Ewe Mola wetu
Mlezi! Tuakhirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume. Kwani
nyinyi si mliapa zamani kwamba hamtaondokewa?
|
Ayah 14:45 الأية
وَسَكَنتُمْ فِي مَسَاكِنِ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ وَتَبَيَّنَ لَكُمْ
كَيْفَ فَعَلْنَا بِهِمْ وَضَرَبْنَا لَكُمُ الْأَمْثَالَ
Swahili
Na mkakaa katika maskani zile zile za walio zidhulumu nafsi zao. Na
ikakudhihirikieni jinsi tulivyo watendea. Nasi tukakupigieni mifano mingi.
|
Ayah 14:46 الأية
وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ
لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ
Swahili
Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu.
Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.
|
Ayah 14:47 الأية
فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ ذُو
انتِقَامٍ
Swahili
Basi usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, na ni Mwenye kulipiza.
|
Ayah 14:48 الأية
يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّهِ
الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ
Swahili
Siku itapo geuzwa ardhi iwe ardhi nyengine, na mbingu pia. Nao watahudhuria
mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mwenye nguvu.
|
Ayah 14:49 الأية
وَتَرَى الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُّقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ
Swahili
Na utaona wakhalifu siku hiyo wamefungwa katika minyororo;
|
Ayah 14:50 الأية
سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ وَتَغْشَىٰ وُجُوهَهُمُ النَّارُ
Swahili
Nguo zao zitakuwa za lami, na Moto utazigubika nyuso zao.
|
Ayah 14:51 الأية
لِيَجْزِيَ اللَّهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ
Swahili
Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale iliyo yachuma. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
|
Ayah 14:52 الأية
هَٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ
إِلَٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ
Swahili
Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni
Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|