Ingia
  Create an account
Ukarasa Yako
Ingia Kati
 
 
 
Kiswahili

- Ukurasa Kuu
- Kumi Juu
- Mada Mpya
- Salimisha Habari
- Tafuta
- Kiswahili Jukwaa
- Kiswahili Wanachama
- Tathmini
- Ujumbe wa Kibinafsi
- Tafiti
- Majarida
- Hadithi Archive
- Maudhui
- Viungo vya Wavuti
- Vipakuliwa
- Maswali ya Kawaida
- Tunapendekeze
- Orodha ya Kuingia


Kubwa Hadithi Ya Leo

Hakuna hadithi kubwa ya leo, bado. Jiunge Sasa!

Idadi Ya Habari Kwa Mzunguko


Ramadhan Eid ul Fitr Eid ul-Adha sikukuu
[ Ramadhan Eid ul Fitr Eid ul-Adha sikukuu ]


Nani Ni Online

Saa hii, kuna hatua ya baraza na wewe mwenyewe 2 Mgeni (wageni) na 3 mwanachama (s) ambayo juu ya Hatua.

Mwanachama (wanachama) pamoja na wanachama wa Awqaf. kuona ni nyingine mbunge (s) online na wewe click Kubonyeza Hapa

Tafuta
Lugha

Mabadiliko ya lugha mbalimbali::


Categories Menu

Hakuna bidhaa sasa hivi kwa ajili ya kuzuia hili.

Sanduku Kuingia

Utani

Siri

Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.

Makala Ya Zamani

Monday, December 03
· Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Saba - Wanaume Na Wanawake Watoao Sadaka
· Umuhimu Wa Kuchunga Wakati
· Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tisa - Wanaume Na Wanawake Wanojihifadhi Tupu
· Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhu
· Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu
· Unavaa 'NIKE', Je, Unajua Maana Yake?
· Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhu
· Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njema
Friday, June 29
· Sha'abaan: Fadhila Zake Na Uzushi Wa Nisfu Sha'abaan - Nasiha Za Minas
· Makatazo Ya Kishari'ah Kwa Wanawake - 5
· Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-3 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah -
· Matayarisho Ya Ramadhaan: Jitathmini Kabla Ya Ramadhaan
· Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 4
· Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd
· Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 3
· Fadhila Za Swawm: Funga inamuokoa mtu kutokana na moto, Swawm ni kinga kutokana
· Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 2
· Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah -
· 'Iyd Taratibu Na Shari'ah Zake: Ahkaamul-'Iyd (Shari'ah Kati
· Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 1
· Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda - Chembe Nyeusi )
Thursday, May 10
· Ukweli Kuhusu Mazishi Ya Kiislamu
· Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?
· Simulizi (Kisa) Ya Hijaab Ya Khawla: Maoni ya Hijaab
· Baada Ya Kuhamia Madiynah: Mwenendo Wa Mitume ('Alayhimus Salaam)
· Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam) Akiwa Madiynah
· Hukumu Za Janaazah
· Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa
· Maovu Yanaofanyika Katika Sherehe Za ‘Arusi (Harusi)
· Isbaal – Vazi La Mwanamme Lenye Kuvuka Mafundo Ya Miguu (Uburuzaji Au Kuburura)
· Wasiya Wa Kishari'ah Wa Muislamu Kabla Hajafariki
· Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawa
· Maslahi Ya Jamii Ndani Ya Shari'ah
· Hijrah: Chanzo Cha Mageuzi
· Yampasayo Maiti
· Hijaab - Kuwajibika Kwake
· Kumtii Allaah Na Mtume Ni Njia Pekee Ya Uongofu
· Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuata Rai Zao
· Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali Kwa jina la Allaah, Mwingi wa Rehma, Mwenye
· Kumpenda Mtume (SAW) Ni Kumtii Na Kumfuata
· Mwito Kutoka Masjidul-Haraam Kwa Wanawake Wote Waislamu Ulimwenguni!
· Mjue Mtume Wako (SAW) Vizuri Uzidi Kumpenda
· Hukmu Ya Kufuga Ndevu
· Kazi Katika Uislam: UTANGULIZI, HADHI YA KAZI, KAZI ZILIZOHARAMISHWA,
Tuesday, October 05
· Ingia Katika Milango Mingi Ya Kheri Ya Ramadhaan
· Tumkumbuke Allaah Sana Na Tuombe Maghfirah Baada Ya Kutenda Mema Katika Siku Kum
· Hajj: Hatua Kwa Hatua: Tazama Televisheni Ya Saudi Arabia kujua wanayofanya Mahu
· Makos Tanayohusu Twawaaf, Sa'y, Yanayotendeka Minaa, Katika Kisimamo Cha &#
Tuesday, May 11
· HADIYTH ARUBAINI ZA IMAAM AN-NAWAWIY NA TAFSIYR YA KISWAHILI
· SUNNAH NZURI KATIKA UISLAM: Jibu la Sheikh 'Abdul 'Aziz bin Baaz

Wazee Makala

Kiswahili

- Ukurasa Kuu
- Kumi Juu
- Mada Mpya
- Salimisha Habari
- Tafuta
- Kiswahili Jukwaa
- Kiswahili Wanachama
- Tathmini
- Ujumbe wa Kibinafsi
- Tafiti
- Majarida
- Hadithi Archive
- Maudhui
- Viungo vya Wavuti
- Vipakuliwa
- Maswali ya Kawaida
- Tunapendekeze
- Orodha ya Kuingia

Manufaa Na Matatizo Katika Ndoa
 
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis Manufaa Na Matatizo Katika Ndoa

Imefasiriwa Na: Ummu Ahmad MANUFAA KATIKA NDOA 1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu.
2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi:
“Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu.” [Ahmad]
3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa:
“Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake.” [Riyadhus-Swaalihiyn]
Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:


4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au yanokaribisha tendo la zinaa.
5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea mapenzi na huruma baina ya mume na mke.
6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni.
7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka, kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza.
8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha, kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.

MATATIZO KATIKA NDOA
Wakati huo huo kuna matatizo yanayopatikana katika ndoa ambayo inabidi tuzingatie na kujichunga ili tuepukane na matatizo hayo. Nayo ni kama yafuatayo:
1. Kushindwa kuchuma pato la halali, ambapo itapelekea kutafuta njia ambazo si za halali za kimapato ili kuweza kutimiza mahitaji ya familia. Haimfalii mke kumlazimisha mumewe ampatie mambo yaliyo nje ya uwezo wa mume. Na tuwaige wanawake wema waliopita, ambao kila waume zao wakitoka kwenda kwenye shughuli zao za kutafuta riziki, wakiwausia kuwa wasirejee na chochote cha haramu. Wakiwanasihi waume zao kuwa ni bora wastahamili kwa njaa ya hapa duniani kwani adhabu ya kesho Aakhirah sio ya kustahamilika.
2. Kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, na hasa kutimiza haki za mke au kutoweza kustahamili kwenye wakati mgumu wa kimaisha. Na tuwe makini katika suala hili kwani kuna ile dhana ya kuwa ndoa ni jambo la kujionyesha tu kuwa fulani kaoa au kaolewa.
“Kila mmoja kati yenu ni mchungaji, na kila mmoja kati yenu atapaswa kuulizwa ya juu ya kile anachokichunga. Mume ni mchungaji wa familia yake, naye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga. Na mke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe, naye pia atapaswa kuulizwa juu ya anachokichunga. Hivyo basi, kila mmoja kati yenu ni mchungaji ambaye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga” [Al-Bukhaariy na Muslim]
3. Kuacha kushughulikia mambo muhimu ya kidini, kwa mfano kutumia muda mwingi katika mambo ya anasa za kidunia kama vile kuangalia Televisheni, kwenda kwenye shehere za kuzaliwa mtoto au kwa kutimiza umri fulani wa mtoto (birthday party), badala ya kutumia muda huo kwa kutengeneza maisha ya Aakhirah ambayo ndio ya milele. Kama tunavyotanabahishwa kwenye Quraan Tukufu:
“Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Allaah. Na wenye kufanya hayo ndio walio katika khasara.” [Al-Munaafiquun 63: 9]

Mwandishi wa mada hii amemalizia kwa kusema kuwa:
Dinaar (pesa) unayoitumia katika njia za Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala), dinaar unayoitumia kumuachia huru mtumwa, dinaar unayoitumia katika kutoa sadaka kwa mtu anayehitaji sadaka hiyo, basi hakuna Dinaar iliyo bora kati ya dinaar hizo ila ile unayoitumia kwa ajili ya familia yako.
Msemo huu una maana ya kwamba hakuna jambo muhimu katika mafundisho ya kijamii ya Kiislamu kama lile la kuzishughulikia familia zetu kwa mali na hali, ili kuweza kupata umma mwema na bora duniani na Aakhirah.

Mwishoni tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Atupe wake, waume na watoto watakaotupa kitulizo cha macho na nyoyo zetu, na Atufanye tuwe viongozi wazuri wa familia zetu. Ee Allaah Mpe Bwana Wetu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Baraka na Amani na Familia yake pamoja pia na Maswahaba wake. “Aamiyn”
 
 
 Posted By Posted juu ya Wednesday, December 19 @ 11:53:09 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: